Masomo

Somo Maelezo Ada

Kuchunguza Maandiko Matakatifu

Kozi hii inaeleza kifupi sehemu za Biblia na kusudi lake.
Somo la kwanza Download PDF
Mtihani Download PDF

0/-

Mungu Mmoja Njia Moja

Kwa mifano ya Agano la Kale na Agano Jipya kozi hii inaeleza jinsi Mungu alivyo na makusudi yake kwa watu wa dunia yetu.

2000/-

Mtumishi wa Mungu

Somo hili linafafanua sehemu ya kitabu cha Injili ya Marko.

2000/-

Mungu

Kozi hii inachunguza maswali yafuatayo:
Mungu ana tabia gani?
Kuna miungu mingapi? Je, Mungu anajulikana?

2000/-

Neno la Mungu

Somo linahusu Injili ya Yohana, yaani kitabu cha nne cha Agano Jipya. Kinachoonesha habari ya Bwana Yesu na maisha yake duniani. Kinatueleza kuwa Yesu ni neno la Mungu na matendo yake aliyotenda. Somo hili likusaidie kumjua Mungu mwenyewe.

2000/-

Njia ya Wokovu

Jinsi ya kuupata wokovu wa Mungu ni jambo gumu linalowasumbua watu wengi sana leo. Kitabu hiki kinaeleza mambo muhimu yanayohusu jambo hili.
Ndani yake kuna mistari iliyonukuliwa kutoka katika Neno la Mungu, yaani Biblia.

2000/-

Chupa12

Mtume Petro aliwaambia Wakristo kuwa lazima wawe kama watoto wachanga na siku zote wawe na kiu ya maziwa safi ya kiroho,
1 Petro 2:2. Maziwa haya ni Neno la Mungu ambalo hutusaidia kukua kama Wakristo.
Kunywa kwa wingi, Mpendwa.
Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema, (Zaburi 34:8).

2000/-

Majuma mawili katika Shule ya Maombi

Kwa mfano wa mtu na mchungaji wake tunajifunza jinsi ya kuzungumza na kumsikiliza Mungu.
Kusudi la somo hili ni kwamba upate kujiendeleza katika mambo ya maombi. Unaposoma habari za watu hawa utajifunza siri chache zilizo muhimu kuhusu maombi yanayojibiwa. Mungu anadhihirisha siri hizi katika Biblia.

2000/-

Maisha ya Mkristo

Masomo ya kitabu hiki yanatufundisha baadhi ya mambo yaliyo muhimu sana katika maisha ya Mkristo. Lakini tutafakari maana ya maneno hayo Mkristo na Maisha. Biblia husema kwamba wanaomwamini Yesu Kristo wana “uzima wa milele,” milele maana yake daima. Mkristo akifa ataendelea kufurahia aina hii ya maisha katika nyumba ya Mungu, mbinguni.

2000/-

Biblia Ifunzavyo

Mafundisho ya msingi kuhusu Biblia, Mungu, dhambi, Wokovu n.k.

2000/-

Mwokozi wa Ulimwengu

Maelezo ya Injili ya Luka.
Somo linahusu maisha ya Bwana Yesu Kristo. Mwandishi Luka aliyekuwa daktari, aliwauliza watu wamwambie yale waliyoyaona na kuyasikia kuhusu Yesu. Kisha akayakusanya yote aliyokuwa na uhakika nayo akiongozwa na Roho Mtakatifu.

2000/-

Mwenendo wa mwamini

Matokeo ya kuzaliwa mara ya pili, uhakika wa wokovu, kushinda majaribu n.k.

2000/-

Waraka kwa Warumi

Waraka huu unaonesha jinsi Mungu anavyokutana na nia mbalimbali ambazo akili za mwanadamu huzifuata katika kuhusiana naye mwenyewe na kweli zake.
Njia rahisi ya kuelewa kitabu hiki ni kukiona kama mfululizo wa maswali na majibu.

2000/-

Je, Twaweza Kumjua Mungu?

Watu wengi hawamwamini Mungu. Wengine huishi tu kana kwamba hakuna Mungu. Wengine husema, labda Mungu yupo lakini hakujionesha kwa wanadamu. Kwanza tutajibu swali lisemalo, “Je, kuna Mungu?” Pia maswali yafuatayo yatachunguzwa: Mungu yukoje? Mwanadamu ni nani? N.k.

2000/-

Wanaume Waliokutana na Bwana

Katika somo hili tumechagua wanaume sita waliokutana na Bwana Yesu katika matukio yaliyohusiana na kifo chake. Walifanya nini watu hao katika wakati huo muhimu? Ndiyo, baadhi yao walitenda kinyume naye; na wengine walimwunga mkono kwa ujasiri. Na sehemu ya yale waliyoyatenda na kuyasema, yameandikwa kwa ajili yetu kwamba tuweke moyoni mafunzo tunayopata humo.

2000/-

Petro na Kanisa

Mafundisho kufuatano na maisha ya Petro uhusiano wake na kanisa.

2000/-

Kukua katika Imani

Hatua zinazosaidia kukua katika Imani na umuhimu wake, k.m. kutubu, kukariri mistari ya Biblia, matendo mema n.k.

2000/-

Roho Mtakatifu na Kazi Yake

Roho Mtakatifu ni nani? Mifano ya kazi za Roho Mtakatifu na nguvu yake.

2000/-

Biblia ni ya Ajabu

Umoja wa Biblia, Biblia ilitokeaje, Kanuni ya Biblia, kuenezwa kwa Biblia duniani. Biblia ni pumzi ya Mungu.

2500/-

Nyaraka za Yohana

Nyaraka za Yohana ni za kiutendaji. Pia zinaweza kushtua, kwa sababu Yohana anazungumzia mambo yote kwa uwazi bila kuficha jambo lolote katika maisha yetu. Mambo hayo yote ama ni meupe au meusi, ni ya kweli au uongo, mema au maovu ameyataja. “Mungu ni nuru, na ndani yake hakuna giza hata kidogo”.
Kwa hiyo nyaraka hizi zinafaa sana kwetu siku hizi.

2500/-

Safari katika Biblia

Somo linaanza na mpango wa Mungu kwa uumbaji. Mpango wa Mungu kwa mwanamume na mwanamke wa kwanza hadi mpango wa Mungu kwa kanisa na hata kwa siku zijazo zinaelezwa na mengine mengi pia.

2500/-

Mambo Yajayo

Bwana Yesu aliwaambia marafiki zake mambo mengi yatakayotokea baadaye. Jambo moja zuri limeandikwa katika Yohana 14:3, “Nitakuja tena”. Yeye alikuwa anaondoka ili awatayarishie mahali na kuahidi kuja tena. Alitaka wawe pamoja naye huko mbinguni. Je, Bwana Yesu yuko wapi leo? Yuko mbinguni, anataka tuwe pamoja naye mbinguni. Sisi hatuwezi kuona njia inayoelekea mbinguni au kufika wenyewe pale, kwa hiyo aliahidi kurudi tena. Huu ni ukweli mkuu wa kwanza ambao inabidi tuufahamu: Bwana Yesu aliahidi kuja tena. Somo linachunguza mambo mengi zaidi kwenye Biblia kuhusu muda ujao.

2500/-

Chakula cha Bwana

Somo linafundisha kuhusu Ushirika wa Chakula cha Bwana na Pasaka, mifano na maana yake, kutimiza agizo, na jinsi ya kujiandaa kwa Ushirika

1000/-

1 Wakorintho

Je, kuwako kwa madhehebu kunaungwa mkono na Maandiko? Kwa sababu ya dhambi gani Mkristo anaweza kutengwa na kanisa lake? Je, ni haki kwa mwamini kumshtaki mwamini mwenzake mahakamani? Ndoa inapewa nafasi gani katika Agano Jipya? Kipawa cha kunena kwa lugha ni nini? Mwili wa ufufuo utakuwaje?
Haya ni baadhi ya maswali makubwa ambayo Paulo anayajibu katika waraka wake wa kwanza kwa Wakorintho.

3000/-

Kuzikwa kwa njia ya Ubatizo

Uchunguzi wa ubatizo katika Agano Jipya na uhusiano wake na imani katika Kristo.

1000/-

Timotheo na Tito

Nyaraka hizi za uchungaji zinafundisha maana ya kanisa la kibiblia, wajibu wa Wakristo, na jinsi inavyopasa kanisa litawaliwe.

3000/-

Kristo alilipenda Kanisa

Kozi hii itakusaidia kwa kuiruhusu Biblia izungumze yenyewe kuhusu swala hilo la Kanisa.
Je, maana ya Kanisa iliyoelezwa katika Agano Jipya ikoje? Ni nini mawazo ya Mungu kuhusu Kanisa? Je, mwanzoni Kanisa lilikuwaje? Na leo Kanisa linapaswa liweje?

2000/-

Uvuvi wa Watu

Mojawapo ya faida kuu za mwamini, yaani mfuasi wa Kristo, ni kuhusishwa na Mungu katika kazi muhimu ya kuwavua watu, yaani kuwavuta kwa Bwana Yesu Kristo waokolewe (Mithali 11:30). Kati ya mambo yatendwayo na wanadamu ni machache tu ambayo matunda yake yatadumu milele. Hakika mtu anayefanya kazi hiyo anajiingiza kwenye mambo ya milele, na thawabu yake itadumu milele (Danieli 12:3).
Kozi hii inachunguza huduma hii kwa upana wake.

2000/-

Ufunuo

Tunaishi katika siku za maana sana.
Je, Biblia inasema nini kuhusu nyakati kama hizi? Je, tunaishi wakati wa siku za mwisho? Je, Biblia inazungumza kwa uhakika na kwa mamlaka juu ya mambo hayo na matatizo ya siku hizi? Je, inaweza kutufunulia mambo yanayopaswa kutokea? Kitabu cha Ufunuo hufunua mambo yatakayotokea.

3000/-

Al-Kitab

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kwa kozi hii ya Biblia.
Mwislamu mashuhuri mtunzi wa mashairi katika karne ya kumi na tatu B.K. (Baada ya Kristo), aliyeitwa Jalul’l-Din huko Rumi alisimulia hadithi ya tembo aliyekuwa katika chumba chenye giza.Baadhi ya watu fulani walimleta tembo huyo Arabuni na wengi wakaenda kumwona. Kwa bahati mbaya chumba alichowekwa kilikuwa na giza sana hata wageni waliofika “walimwona” kwa kumgusa tu. Mmoja wao aligusa mkonga wa tembo na aliamini kuwa tembo ni kama mwanzi. Mwingine aligusa sikio na alisema amefanana na kipepeo. Wengine walibishana kuwa amefanana na ukuta, maana waligusa ubavu, wengine shina la mti, maana waligusa mguu, wengine kamba, maana waligusa mkia, na kadhalika. Kila mmoja wao alikuwa na sehemu ndogo ya ukweli lakini hakuna hata mmoja aliyejua kwa hakika tembo amefanana na nini.
Kozi hii ya Biblia imetayarishwa ili kuwasaidia Waislamu kumjua “tembo” wa Biblia kama tunavyoona katika hali yake ya mwanzo katika Al-Kitab ama kwa ukweli Al-Kutubul-Muqaddas, “Maandiko Matakatifu”, yaani Biblia. Na kozi hii inaweza kusaidia kuzungumza kuhusu habari ya Biblia.

3500/-

Matendo ya Mitume

Kitabu cha Matendo kinatusimulia jinsi kanisa la kwanza lilivyolikabili Agizo Kuu la Bwana. Kinatuambia jinsi Injili ilivyoenea magharibi na hatimaye kuingia katika jiji la Rumi. Kitabu hiki kinasimulia juu ya watu na pia sehemu mbalimbali. Kinadhihirisha kanuni za mipango makini ya kupeleka injili katika pande zote za ulimwengu.
Masomo ya kitabu hiki kwa ujumla ni rahisi, hata hivyo yanaleta changamoto kubwa. Lengo la masomo haya ni kutazama matukio yanayosisimua, ambayo yalibadili kabisa historia ya nyakati zote zilizofuata. Tunatumaini kwamba yatakupa changamoto na pia baraka kwako.

3500/-

Jifunze Biblia Nzima

Mafunzo haya yanaeleza kwa muhtasari vitabu vyote vilivyomo katika Biblia. Mambo hayo yote yameoneshwa katika nyakati zake, mahali pake pamoja na maelezo mafupi.

3500/-

Kitabu cha Mwanzo

Kitabu cha Mwanzo ni msingi na mahali pa kuanzia ujumbe wa Neno la Mungu zima. Ukitaka kuelewa vitabu vyote vya Biblia inakupasa ujue kitabu cha Mwanzo.

3500/-

Injili ya Marko

Marko aliandika Injili hii kwa ajili ya mtu wa kawaida.
Katika Injili hii tunapata habari njema kuhusu Mtumishi Mkamilifu wa Mungu, Bwana wetu Yesu Kristo. Hizi ni habari za yule aliyeweka kando utukufu wake wa mbinguni na kuvaa hali ya utumishi wa hapa duniani (Wafilipi 2:7).
Tunapochunguza Injili hii tutazingatia maswali matatu yafuatayo:
1. Je, inasema nini?
2. Je, inamaanisha nini?
3. Je, mimi ninapata fundisho gani?
Kwa watu wote walio na nia ya kuwa watumishi waaminifu wa Bwana, Injili hii itakuwa msaada kabisa.

3500/-

Njia ya Kutoka na Kuingia

Kitabu cha Mwanzo kinaishia na habari ya kufa kwa Yakobo katika nchi ya Misri.
Kitabu cha Kutoka kinaendelea na historia ya watu waliochaguliwa. Mfalme mpya wa Misri aliwafanya kuwa watumwa. Kitabu cha Kutoka kinaeleza jinsi Mungu alivyowaongoza watu wake kutoka Misri na kuingia jangwani. Neno “Kutoka” maana yake “Njia ya Kutoka”. Tutachunguza kitabu cha Kutoka kwa makini na pia kitabu cha Mambo ya Walawi ambacho ni vigumu sana kuelewa bila maelezo. Pia somo hili linalinganisha mistari ya Biblia sehemu ya Agano la Kale na Agano Jipya zenye maana moja.

3500/-

Safari Jangwani

Vitabu vya Hesabu na Kumbukumbu la Torati ni sehemu muhimu za Neno la Mungu. Kama ukielewa kitabu cha Hesabu na cha Kumbukumbu la Torati, utaweza kuelewa vizuri zaidi sehemu nyingi za Biblia. Pia utaelewa zaidi kuhusu Mungu pekee wa kweli. Pia somo hili linalinganisha mistari ya vitabu hivi na Agano Jipya na kueleza zinatokea wapi katika Agano Jipya na kwa tukio gani.

3500/-